News

Wajibu wa kujenga Nyumba za Wachungaji wa Mitaa

Ujenzi wa Nyumba za mitaa kwaajili ya Wachungaji ukiendelezwa katika mitaa yote katika kanisa la Waadventista wa Sabato kote katika majimbo yote ndani na nje ya Jimbo kuu la Kaskazini mwa Tanzania utaokoa fedha nyingi zinazotumiwa kwaajili ya kulipia pango katika nyumba wanazoishi Wachungaji.

Haya yamesemwa na Mch na Dr. Godwin Lekundayo, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Kanisa la Waadventista wa Sabato, wakati akiweka Jiwe la msingi la nyumba ya Mtaa ya Mchungaji katika Mtaa wa Heri Wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

Aidha Amewapongeza washiriki kwa kujenga Nyumba nzuri ya mtaa kwaajili ya Mchungaji inayomtukuza Mungu nahivyo kupunguzia konference pesa nyingi wanazo toa kila mwezi

Dr. Lekundayo ametoa wito kwa Washiriki katika mitaa mingine kuiga Mtaa wa Heri katika Wilaya ya Buhigwe mkoani Kin go ma kwakuwa kielelezo kwakujenga nyumba nzuri kwaajili ya mtumishi wa Mungu

Nae Mchungaji Benadi Mabwe Mwenyekiti wa jimbo Dogo la Magharibi mwa Tanzania amesema kuwa Idadi ya Nyumba Zilizopo za Mitaa kwaajili ya wachungaji ni 37 na Uhitaji ni Nyumba 24 na kila mwezi conference humia shilingi 4,513,750 kwaajili ya kulipia Pango kwaajili ya yumba wanazoishi Wachungaji na Idadi ya Wachungaji kwasasa ni 65 hivyo wachungaji 24 wanaishi katika nyumba ambazo sio za kanisa nakuligharimu Kanisa

Hivyo amewapongeza Mtaa wa Heri kwa jitihada za makusudi walizozifanya kupunguzia jimbo la Magharibi gharama za pango katika mtaa huo.

 


One comment

  • | 5 years ago

    I have not checked in here for a while as I thought it was getting boring, but the last several posts are good quality so I guess I¦ll add you back to my daily bloglist. You deserve it my friend 🙂

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *